Thursday, 10 March 2016

PICHA: MAZISHI YA SHEIKH MUHAMMAD BAKAR TANGA

Mwili wa Mwanazuoni mkubwa ukanda wa Afrika Mashariki Sheikh Muhammad Bakar Al- burhan, Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya Tanga umezikwa jana katika viwanja vya chuo hicho.

Maelfu ya waumini kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi walijitokeza kuusindikiza mwili wake.

Shughuli za mazishi zilianza mapema kwa Masheikh mbalimbali kuelezea wasifu wa ilmu yake na uchaungu wake.
Naib Mudir Sheikh Samir Sadiq na Ustaadh Rashid Bakar wakipanga ratiba
Waliongia kaburini ni Ustaadh Rashid Bakar, Abdulhamid Muhamad Bakar,Sharif Hussein Hashim, Sharif Haidar 'Dogo', Ustaadh Yusuf Kidago na Ustaadh Hussein Abbas.
Umati wa waumini wakisikiliza wasifu wa Sheikh Muhammad Bakar
Sharif Mihdhwar Khitamy akizungumza
Sharif Hussein Hashimu Akizungumza
Waumini wamejipanga kwa ajili ya Jeneza
Tayari kaburi likiwa lishachimbwa
Mwili wa Sheikh ukitolewa nyumba kwake na kupelekwa madrasa