Tuesday, 8 March 2016

MWILI WA SHEIKH MUHAMMAD BAKAR WASAFIRISHWA LEO KUELEKEA TANGA KWA MAZISHI

Mwili wa Mwanazuoni mkubwa ukanda wa Afrika Mashariki Sheikh Muhammad Bakar Al- burhan, Mudir wa Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif ya Tanga umesafirishwa Leo saa saba za mchana kuelekea Tanga kwa ajili ya maziko.

Mwili wake umesafirishwa kwa ndege ukiambatana na baadhi ya wanafamilia na watu wa karibu wapatao 12.

Sheikh atazikwa kesho wakati wa alasiri katika viwanja vya Mahdi(chuo kikuu) Shamsul Maarif mtaa wa duga jijini Tanga.
Wageni mbalimbali kutoka sehemu kadhaa za ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.