Monday, 28 March 2016

MASAA MACHACHE YA KUFUNGA RAMADHANI NEW ZEALAND KUVUTIA WATALII WA KIISLAMU

Muda wa kufunga mwezi wa Ramadhani utakuwa kwa masaa machache huko New Zealand hivyo kuvutia watalii wa kiislamu kwenda kwa ajili ya kufunga ndani ya mwezi huo amesema mkuu wa taaluma wa chuo kikuu cha Auckland Dr. Zain Ali.

Mfungo wa Ramadhani New Zealand unatarajiwa kuanza Mwezi Juni tarehe sita kutegemea na mwandamo wa mwezi.
Waislamu wakisali msiki wa Hawke's bay and Islamic Centre
Waislamu wanatarajia kufunga kwa muda wa masaa 11 kila siku na kuwa sehemu ya wafungaji wake kufunga masaa machache zaidi kuliko sehemu nyingine.

Baadhi ya nchi za Ulaya wanatarajia kufunga takribani masaa 20 au masaa 15 katika nchi za mashariki ya kati.

Dr. Zain Ali ambaye ni mkuu wa utafiti wa Kiislamu alisema kuwa kwa mazingira hayo yanaipa New Zealand nafasi nzuri ya kupokea watalii wengi wa kiislamu katika mwezi huo Mtukufu. 

Mwezi wa Juni ni kipindi cha baridi hivyo masaa ya mchana hupungua huko New Zealand.