Mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qurani nchini Singapore yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika siku ya jumamosi na jumapili ya Mwezi April tarehe 2-3.
Makundi matatu yatakayoshiriki ni ya Umri wa miaka 7 mpaka 12, miaka 13 mpaka 18 na miaka 19 mpaka 25.
Washiriki hao watashindanishwa kwa kuzingatia namna walivyohifadhi (Hifz), matamshi (Tajweed), na ufasaha (Fasahah).
Lengo kuu la mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya katika uwanja wa usomaji wa Qurani na kuhamasisha kuhifadhi Qurani.
Aidha lengo lingine ni kuifanya jamii kuwa na utamaduni wa kuhifadhi Qurani na pia kupata vijana watakaoiwakilisha Singapore katika mashindano ya kimataifa.
Mashindano hayo yatafanyika katika Msikiti wa Darul Aman na washindi watapata vyeti na pesa taslimu.
