Tuesday, 22 March 2016

ASKOFU APINGA WAISLAMU KUSALI NDANI YA KANISA, MAKUHANI WARUHUSU WAENDELEE NA IBADA

Askofu Mkuu Fausto Tardelli wa kanisa la Vicofaro, Pistoia, Toscana nchini Italia, amewapigia kelele mapadri wawili wa kanisa hilo kwa kuwaruhusu wakimbizi wa kiislamu kufanya ibada ndani ya kanisa hilo.

Baba Massimo Biancalani na Alessandro Carmignani walitangaza wiki iliyopita kuwaruhusu kusali waislamu ndani ya kanisa baada ya parokia yao kuwakaribisha wakimbizi 18 waislamu.
Waislamu wakisali ndani ya kanisa
Massimo Biancalani alisema waliondoa vikalio katika altari ili kuwasaidia wakimbizi hao wa kiislamu kujihisi wapo nyumbani.

"Sioni ni jinsi gani tatizo, tunaweza kuwatia ugumu kufanya ibada zao", alisema na kuongeza, "Mtu yeyote akitaka kuja kusali Kanisani anakaribishwa na hata kama wanataka kwenda sehemu nyingine wanaruhusiwa kufanya hivyo".

Lakini Askofu Mkuu Fausto Tardelli alisema mpango huo ni hatua ya mbali ambayo inaweza kuhatarisha na kuharibu kuwaunganisha wakimbizi hao katika jamii. 

Alisema kuwapa misaada na kuwakaribisha haina maana kuwapatia nafasi katika Kanisa kufanya ibada zao. Kuna maeneo bora sahihi zaidi yanapatikana.

Pamoja na kupinga kwa Askofu mkuu wa Kanisa hilo Makuhani wa kanisa hilo wamepinga vikali kauli ya Askofu na kutaka wakimbizi hao waendelee kufanya ibada zao
kanisani hapo na kutaka Parokia zingine ziige mfano wao. 

JE, uislamu unasemaje juu ya kusali ndani ya kanisa?
Fuatilia hapa hapa katika Blogu yako Ahbaabur Rasuul kupata majibu.