Taasisi ya kwanza ya kibenki inayofuata kanuni za kiislamu inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Machi katika mji wa Kazan nchini Urusi.
Taasisi hiyo 'The Partnership Banking Center' itafanya kazi kama kampuni tanzu ya Tatagroprombank alisema mmoja wa waanzilishi wa taasisi hiyo.
Taasisi hiyo itafanya kazi na watu binafsi na makampuni mbalimbali. Aidha itakuwa na lengo la kupitishia uwekezaji wa kiislamu katika nchi ya Urusi.
Pia itasaini makubaliano ya kikazi na Benki ya maendeleo ya kiislamu Islamic Development Bank.
Hili limekuja baada ya upitishwaji wa sheria mpya katika jimbo la Duma mwezi Januari mwaka huu ya kuruhusu mfumo wa kibenki unaoweza kuzingatia taratibu za kidini.
