Tuesday, 2 February 2016

RAIS OBAMA KUZURU MSIKITI NCHINI MAREKANI, NIA NI KUPUNGUZA NA KUTETEA UHURU WA KUABUDU

Kwa mara ya kwanza rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kufanya ziara katika msikiti akiwa rais wa Marekani.

Rais Obama atazuru msikiti kwa niaba ya kutetea uhuru wa kuabudu.


Taarifa kutoka White House zinafahamisha kuwa ziara hiyo ya rais Obama inafuatiwa na ongezeko la vitendo ikiwemo matamshi yasioridhisha dhidi ya uislam na waislamu.

Rais Obama atazuru msikiti wa Islamic Society unaopatikana Baltimore ifikapo Alhamis Juma lijalo.