Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salum alisema njia pekee ya kuleta suluhu Zanzibar ni kwa vyama vyote kukubali kushiriki uchaguzi huo wa marudio.
Sheikh Alhad alisema kwamba ameandikiwa barua na Sheikh Farid ambaye ni kiongozi wa uamsho kwamba ameafiki hakuna njia zaidi ya kurudia uchaguzi.
![]() |
| Sheikh Alhad Mussa Salum |
"Namshukuru sana kwa kuona jambo hilo kwamba solution ya Zanzibar, watu ni kurudia uchaguzi. Hivyo basi naomba kuchukua fursa hii kukiomba chama cha CUF ambacho tayari kimetangaza kususia uchaguzi huo na vyama vingine vilivyopo Zanzibar vione umuhimu wa Zanzibar kuileta pamoja kwa wao kukubali kushiriki uchaguzi huo", alisema Sheikh Alhad.
Chama cha Wananchi cha CUF tayari kilishatoa tamko la msimamo wao wa kutoshiriki uchaguzi huo.
Uchaguzi wa Zanzibar ulifanyika Oktoba mwaka jana lakini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar ZEC Jecha Salum Jechaalitangaza kuufuta kwa madai ya kwamba uliingia kasoro kadhaa ambapo kulizua mtafaraku wa kisiasa visiwani humo.
Uchaguzi huo umetangazwa kurudiwa tena mwezi Machi 20 mwaka huu.
