Makaburi 6 ya Waislamu yaliyokuwa katika eneo la Seine et Marne kusini mashariki mwa Paris yameripotiwa kuharibiwa.
Meya wa manispaa ya mji wa Dammarie-Les-Lys uliokuwa na makaburi hayo Gilles Battail, alitoa maelezo na kuarifu kwamba makaburi hayo yalichafuliwa kwa rangi nyekundu usiku wa Jumamosi.
Battail alikemea tukio hilo na kufahamisha kuwa wameripoti kwa ofisi husika za mamlaka.
Mkuu wa muungano wa kutetea haki za Waislamu nchini Ufaransa Abdallah Zekri, alilaani tukio hilo na kusema kuwa linavuruga utamaduni wa jamii.
Waislamu nchini Ufaransa wamekuwa wakishambuliwa kwa njia tofauti tangu kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa tarehe 13 Novemba 2015 mjini Paris.
