Monday, 8 February 2016

MJUKUU WA NELSON MANDELA AFUNGA NDOA YA KIISLAMU BAADA YA KUSILIMU

Mandla Mandela ambaye ni mjukuu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela amefunga ndoa ya kiislamu katika mji wa Cape Town mwishoni mwa wiki.

Mjukuu huyo wa Mandela amemuoa Bi Rabia Clarke siku ya Jumamosi na kufanya sherehe Jumapili jioni.

"Nina fahari na furaha kutangaza ndoa yangu na Rabia Clarke iliyofanyika tarehe 6 februari 2016 katika mji wa Cape Town", alisema katika taarifa yake.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wazazi wa Rabia, jamaa zake na jamii ya Waislamu, kwa kunipokea kwa dhati katika dini. Ingawa mimi na Rabia tumelelewa katika mila tofauti za kitamaduni na kidini, lakinindoa yetu inaonesha sisi ni watu wa kawaida. Sisi ni Waafrika Kusini", alisema.

Kwa mujibu wa Channel ya Islam International, Mandla ambaye ni chifu mkuu wa Mvezo, amesilimu miezi miwili iliyopita.

Ndoa (Nikah) ilifanyika katika msikiti wa Kinsington asubuhi ya Jumamosi.