Sunday, 3 January 2016

RAIS WA UTURUKI AMALIZA IBADA YA UMRA

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdogan ametekeleza ibada ya umra akishirikiana na viongozi wengine ambao walikuwa katika ziara nchini Saudi Arabia.
Rais Erdogan alipokelewa na mfalme wa Saudi Arabia Salmane Ben Abdulaziz na baadae kuanza ibada ya Umra mjini Makka.

Rais Erdogan alizuru 'Masjid al-Haram' kwa kupita sehemu kadhaa.
Rais Erdogan alishirikiana katika safari yake hiyo na mkewe Bi Emine Erdogan, waziri wa mambo ya nje Mevlut Cavusoglu, waziri wa mali ya asili Berat Albayrak na waziri wa uchumi Mustafa Elitas.