Nchi tatu zenye maadili ya Kiislamu zimetangaza kuwekea wananchi wake marufuku ya sherehe za mwaka mpya.
Nchi hizo zilizochukuwa uamuzi huo wa kuzuia sherehe za mwaka mpya ni Brunei na Tajakistan kutoka bara la Asia, na Somalia kutoka bara la Afrika.
Sultan Hassanal Bolkiah wa Brunei, alitangaza marufuku hayo kutokana na kuwa kinyume na maadili ya Kiislamu, na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 5 gerezani kwa raia watakaokiuka sheria.
Wizara ya elimu ya Tajakistan nayo ilitangaza kuweka marufuku ya miti ya mapambo ya Krismasi na sherehe za mwaka mpya ingawaje adhabu ya washerehekeaji haikubainishwa.
Kwingineko katika nchi ya Somalia, sherehe za Krismasi na mwaka mpya pia zilipigwa marufuku kwa madai ya kuwa ni misingi ya dini ya Kikristo.
Kiongozi mmoja wa wizara ya masuala ya dini Mohammed Hayrow, alitoa maelezo na kusema kwamba watazuia sherehe zozote zitakazofanyika kwa ajili ya Krismasi au mwaka mpya.
