Wednesday, 13 January 2016

MBWANA SAMATTA AKUTANA NA MUFTI WA TANZANIA, AOMBEWA DUA NA KUPEWA NASAHA ZA KUMCHA MUNGU

Juzi tarehe 11 January 2016, Mwanasoka Bora Afrika Mbwana Ali Samatta alimtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir katika ofisi kuu za Bakwata zilizopo Kinondoni Jijini Dar Es Salaam.

Mbwana samatta mbali na kupatiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa Mufti kwa ajili ya kumsaidia katika imani yake pia alipata nafasi ya kuombewa dua ya mafanikio zaidi huko aendako Ulaya.
Aidha Mufti alimpa nasaha kuwa asisahau kumuomba Mwenyezi Mungu kila wakati na kufanya ibada muda wote atakaokuwa nje ya mazoezi.

Mwisho Mufti alimtakia mafanikio mema na kumuambia dua za watanzania wote zipo naye.