Monday, 28 December 2015

MSIKITI WACHOMWA MOTO TEXAS

Msikiti mmoja mjini Texas nchini Marekani  umechomwa moto na wahalifu wasiojulikana.

Polisi nchini Marekani imesema kuwa wahalifu ambao bado hawajapatikana ndio walioendesha kitendo cha uharibifu dhidi ya mskiti mmoja katika jimbo la Texas.
Moto ulizuka katika jengo la msikiti unaopatika katika kituo kimoja cha biashara katika mji wa Houston.

Baada ya taarifa kutolewa kikosi cha askari wazima moto kiliwasili kabla ya moto huo kuzagaa katika mskiti huo.