Friday, 25 December 2015

KICHWA CHA NGURUWE KILICHOFUNIKWA NA KURASA ZA QURANI CHATUPWA MSIKITINI UJERUMANI

Kichwa cha nguruwe kimepatikana kikiwa kimefunikwa na kurasa za Qurani ndani ya mfuko katika msikiti mmoja mjini Berlin nchini Ujerumani.

Kichwa hicho kimepatikana katika eneo ambalo lina wakazi wengi wa asili ya kituruki katika mji wa Kreuzberg ndani ya msikiti unaoitwa Mevlana katika mji huo.
Polisi mji Berlin imefahamisha kuanzisha upelelezi ili kuwatia mbaroni waliohusika na kitendo hicho.