"Lengo kuu la mkutano huu ni kuwa na msimamo wa pamoja kuelekea watu wasio na dini wa Al-Shabaab na kuwaonesha watu wa Somalia na watu wa dunia kwamba watu hawa wako kwenye njia isiyo sahihi," alisema Ahmed kwenye taarifa yake.
Ahmed alisisitiza jukumu muhimu la maulamaa kwenye kupambana na itikadi ya Al-Shabaab. "Nyinyi ni sehemu muhimu ya utawala kwa taifa hili na mna jukumu kubwa katika mapambano dhidi ya Al-Shabaab," aliwaambia maulamaa hao.
Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Maulamaa wa Somalia, Nor Barud, aliukaribisha uamuzi huo wa serikali.
"Huu ni wakati tete sana kubainisha kile kisicho sahihi na kilicho sahihi, viongozi wa kidini ni viongozi wa watu hivyo lazima tuweke bayana masuala ya kidini ya nchi hii," alisema Barud.
"Al-Shabaab wanadai kuwa wanafuata dini lakini kuuwa watu wasiokuwa na hatia kwenye maeneo matakatifu kama vile misikitini kunaonesha kuwa wao si Waislamu wa kweli wanapotoshwa. Wana uelewa mdogo sana wa kile dini ya Kiislamu inachotufunza."
![]() |
Waziri Mkuu wa Somalia, Abdiweli Sheikh Ahmed |