Tuesday, 18 March 2014

MAKACHERO WAPEKUWA NYUMBANI KWA RUBANI WA NDEGE ILIYOPOTEA YA MH370, MALAYSIA

Polisi nchini Malaysia wamevamia nyumba aliyo kuwa akiishi rubani wa ndege iliyo potea na kuendesha msako mkali,ikiwamo kukufanya nyaraka muhimu ambazo zitawa saidia kufichua ukweli kuhusu tukio la kupotea kwa ndege hiyo.

Ripoti zinasema upekuzi huo ambao pia umefanyika katika nyumba ambayo alikuwa akiishi rubani msaidizi, baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa rubani huyo Zaharie ahmad Shah alikuwa na mlengo wa siasa Kali.

Shah alikuwa ni shabiki na mfuasi wa wazi wa mwanasiasa wapinzani Anwar Ibrahim baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na vitendo vya Fedheha.

Inaaminika kuwa rubani huyo alikuwepo mahakamani wakati mwanasiasa huyo anapandishwa kizimbani mwezi mach mwaka huu na pengine hakufurahishwa na hukumu hiyo.
Kwa sasa polisi wanashikilia nyaraka kadhaa ikiwamo kompyuta inadhaniwa kuwa na taarifa muhimu zilizo hifadhiwa na rubani huyo.

Polisi hao wameenda mbali zaidi na kuanzisha uchunguzi wa kimazingira ambao utawasaidia kupata historia binafsi kuhusu maisha ya rubani huyo,aliye tajwa kuwa na uzoefu mkubwa wa kurusha ndege.

Wataalamu wa saikolojia na wale wanao husika na usalama wa anga wameitwa kuongeza nguvu ili kusaidia kuchambua taarifa zinazo endelea kukusanywa kuhusu mwenendo wa rubani Shah ambaye nyumba yake bado inaendelea kulindwa.

Kitendo cha polisi kufanyia uchunguzi nyumba ya rubani huyo ni pamoja na kukusanya taarifa zake binafsi, imeelezwa kuwa ni jitihada za serikali kutaka kujiridhisha hasa kutokana na mazingira yanayohusu upotevu wa ndege hiyo.

Wachunguzi hao wanataka kujua kama kumekuwa na tukio lolote la matatizo ya kiakili na kumewahi kujitokeza changamoto za kifamilia kwa marubani hao, au kwa yoyote aliye kuwamo ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Kaula Lumpur kuelekea Beijing.

Pamoja na kwamba marubani wa Malaysia walikuwa na rekodi nzuri, kuna wasiwasi pengine walikuwa na tukio lililo sababisha kujiingiza kwenye hali ambayo imepoteza umakini wa kuongoza ndege.

Uchunguzi unao walenga abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo iliyo kuwa na miaka 11 na kwamba inaweza kusaidia upatikanaji wa ukweli halisi juu ya ndege hiyo.

Malaysia imeomba msaada zaidi kutoka nchi kadhaa kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo ya abiria iliyo potea kwa zaidi ya wiki moja iliyopita huku kukiwa na taarifa za kusitishwa uchunguzi kwenye bahari ya Hindi mpaka pale tathimini ya kina itakapo fanyika.

Wizara ya uchukuzi imesema kwamba imeomba msaada nchi za Kazakhistan,Uzbekistan,Kygyzistan,Turkmenistan,na Pakistani.

Nchi nyingine zilizoombwa kushiriki ni pamoja na Indonesia, Thailand,Marekani Australia na Ufaransa.

Msaada huo ni pamoja na takwimu za satelaiti zilizo nasa safari hiyo iliyo kuwa na watu 239 na ambayo ilipotea mach 8 mwaka huu baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Kaula Lumpur.

Awali waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak, alisema kuwa wachunguzi waligundua kwamba ndege hiyo iliyo kuwa ikielekea Beijing nchini China ilibadili njia na kuelekea Magharibi kabla ya mitambo ya mawasiliano yake kuzimwa.

Alizungumza na mwandishi wa habari katika mji mkuu wa Kaula Lumpur Najib Razak alisema
"Wachunguzi wanaamini kwa kiwango kikubwa kwamba kulikuwa na kitendo cha makusudi kuzima mfumo wa mawasiliano katika ndege aina ya Beijing 777-200ER ya shirika la Malaysia airlines. Kwa msingi huo ndege hiyo haingeweza kuwasiliana na kituo cha kudhibiti trafiki angani".

Waziri mkuu wa Malaysia aliongeza kuwa baada ya kuzimwa mfumo huo wa mawasiliano ndege hiyo ili badilisha mkondo wake na kuelekea upande wa Magharibi baharini jambo ambalo lilikuwa na hatua za makusudi.

Alisema pamoja na kuwepo kwa taarifa ndege hiyo ilitekwa bado hakuna lolote lililo wazi ni kwa nini ndege hiyo ilichepuka kutoka katika mkondo wa safari yake.

Pamoja na ukweli kuwa nchi kadhaa zinahusika katika juhudi za kuitafuta kwa kutumia teknolojia ya kisasa bado haijatangazwa kama ndege hiyo iliyotengenezwa marekani imepata athari gani.


Nyumba ya rubani