Wito huo umetolewa na kiongozi katika jimbo la Borno Abubakar Ibn Garbai Elkanemi kwa kuwataka wananchi wote wa Nigeria kumlilia Mwenyezi Mungu kwa kuliangamiza kundi hilo.
"Naamini na tunapaswa kutafuta nusra ya Mwenyezi Mungu ili aturejeshee amani katika jimbo letu", alisema Abubakar.
Aidha aliwataka wananchi kufanya maombi maalumu katika majumba yao ya ibada hata baada ya kufunga kwa muda wasiku tatu. Funga hiyo maalumu ilianza siku ya jumanne na kutarajiwa kumalizika leo siku Alhamis.
Kundi la Boko Haram limekuwa likilaumiwa kwa vitendo vya mauaji ya kikatili pamoja mashambulizi katika majumba ya ibada na mashuleni hususani maeneo ya kaskazini mwa Nigeria katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa.
