Thursday, 13 March 2014

WANAWAKE ALGERIA WAMJIA JUU WAZIRI, KISA KUWATAKA WASIVAE HIJABU MAENEO YA KAZI

Wanawake wa nchini Algeria wamemjia juu waziri wa Mambo ya dini wa nchi hiyo Abu Abdullah Gulamullah kwa kauli yake kuwa wanawake lazima wafuate sheria za kazi kwa kutokuvaa kuvaa Hijabu katika maeneo ya kazi.

Kauli hiyo aliitoa siku ya jumapili kwa kuwataka wanawake wa nchi hiyo kuheshimu sheria katika sehemu za kazi.

Aidha wanawake wamemtaka waziri huyo kufuta kauli yake na akatubu kwa mola wake kwa kutaka kuwazuia na utekelezaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu.

Japokuwa hakuna sheria inayoruhusu wanawake kuvaa hijabu katika maeneo ya kazi, uvaaji wa hijabu kwa wanawake Algeria ni jambo la kawaida.

Wanawake nchini Algeria