Kukamatwa kwa imamu huyo ni kuashiria kwa serikali ya Tunisia kukabiliana na juhudi za kudhibiti misikiti nchini humo.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa umoja wa viongozi wa kidini, Abdessalem El Atoui kwamba Imamu El Merji hakuwa miongoni sehemu ya kundi la masheikh waliopitishwa na serikali kuwa na haki ya kutoa mahubiri msikitini.
Aidha aliongeza kusema kuwa si haki kwa serikali kuwa na mamlaka ya kupitisha nani atoe mawaidha na nani asitoe kwa kufanya hivyo ni kuingilia masuala yasio wahusu tena ya dini.
Serikali ya Tunisia imekuwa ikiorodhesha Maimamu na wahubiri kwa ajili ya kudhibiti wale watakao kuwa wanaikosoa serikali ya nchi hiyo.
Juni mwaka jana serikali iilitangaza misikiti 76 kuwa chini ya muongozo wake. Gazeti la Assabah wiki iliyopita lilimnukuu Waziri wa Mambo ya Kidini Mounir Klibi kwamba sasa serikali imeorodhesha misikiti 149 iliyo chini ya muongozo na maelekezo ya seikali.
