Wednesday, 12 March 2014

AUSTRALIA YAAHIDI DOLA MILIONI 9 KUSAIDIA AMISOM, SOMALIA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Julie Isabela Bishop alitangaza Jumatatu kwamba serikali yake imeahidi dola milioni 9 kama msaada kusaidia Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) na jitihada za kibinadamu katika nchi.

Australia itatoa dola milioni 1.8 kusaidia malengo ya AMISOM, ambalo linapambana na Al-Shabaab pamoja na Jeshi la Taifa la Somalia.

"Dola nyingine milioni 7.2 zitatolewa kama msaada wa kibinadamu kutoa msaada wa kuokoa maisha, kama vile upatikanaji wa maji na huduma za matibabu, na kusaidia kujenga uthabiti wa dharura zinazohusiana na migogoro na hali asili," serikali ya Australia ilisema katika taarifa.

"Itasaidia kukabili ugaidi, kuongeza utulivu katika Ukingo wa Bahari ya Hindi na kupunguza uharamia kando kando ya njia muhimu za biashara kwa ajli ya Australia," Julie alisema katika taarifa kwa mujibu wa gazeti la The Australian.

Julie Isabela