Wednesday, 26 March 2014

WABUNGE WA ETHIOPIA KUPITISHA MSWADA MKALI DHIDI YA MASHOGA

WABUNGE nchini Ethiopia wanatarajiwa kupitisha mswada wa kuorodhesha ushoga kuwa ni miongoni mwa mashtaka yasiyoweza kusamehewa.

Hatua hiyo iliyopendekezwa wiki iliyopita na Baraza la Mawaziri la Ethiopia, inatarajiwa kupitishwa kwa kupiga kura.

Ethiopia ndoa za jinsia moja ni haramu na wanaopatikana na hatia hufungwa miaka 15 gerezani. Kifungo cha miaka 25 pia hupewa mtu yeyote anayemuambukiza mwingine kupitia kufanya ngono na mtu wa jinsia sawa na yake.

Rais wa Ethiopia Mulatu Teshome huwapa msamaha maelfu ya wafungwa raia wa nchi hiyo kila sikukuu ya Mwaka Mpya. Mswada huo ukiwa sheria, rais atapoteza mamlaka ya kuwasamehe wafungwa waliokabiliwa na mashtaka ya ushoga na pia ugaidi.

Ushoga umeharamishwa katika nchio nyingi za Afrika.

Mulatu Teshome, Rais Ethiopia