Wednesday, 26 March 2014

MAHAKAMA YA LIBYA KUSIKILIZA KESI ZA WATOTO WAWILI WA GADDAF MWEZI APRIL

Msemaji wa idara ya uendeshaji wa mashtaka ya Libya amesema, kesi za watoto wawili wa kiongozi wa zamani Muammar Gaddafi na maofisa waanadamizi wa utawala wa Gaddafi, zitasikilizwa kuanzia tarehe 14 Aprili.

Msemaji huyo pia amesema, kesi za maofisa zaidi ya 30, wakiwemo mkurugenzi wa zamani wa idara ya ujasusi na waziri mkuu wa zamani pia zitasikilizwa. Maofisa hao wanakabiliana na mashtaka ya mauaji, utekaji nyara, uporaji, ufisadi na kuharibu umoja wa taifa.

Watoto hao wa Gaddaf ni Saif al Gaddafi na Saad Gaddafi.

Saaad Al Gaddaf
Saif Al Gaddaf