Thursday, 27 March 2014

UINGERZA YARUHUSU SHERIA YA MIRATHI YA KIISLAMU KUTUMIKA NCHINI HUMO

Kwa mara ya kwanza Serikali ya Uingereza itaanza kutambua sehemu ya Sheria za Kislaam kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo.

Gazeti la the Daily Telegraph linalotolewa mjini Landon limemnukuu mmoja wa afisa wa Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Uingereza kuwa Ufalme wa Uingereza umeheshimu na kukubali kanuni ya Sheria za Kiislamu zinazohusiana na Mirathi.

Mwasheria Mkuu wa Uingereza anatarajiwa kutangaza rasmi kwa Waislamu wanaoishi nchini Uingereza kuhukumiwa kwa Sheria hiyo ya kiislamu. 

Gazeti la The Daily Telegraph limemnukuu Nicholas Flock Mkuu wa Wanasheria nchini Uingereza akisema kuwa "Sheria ya Uingereza imekubali sehemu moja wapo ya Sheria za Kislaam kutumika nchini ambayo itawahusu Waislaam tu na ni hatua nzuri kwa jamii ya waishio nchini Uingereza".

Kwa mujibu wa mwanasheria huyo waislamu nchini humo watahukumiwa kwa sheria ya kiislamu katika masuala ya Mirathi na si kwa sheria za uingereza.

Hatua hiyo isiyo ya kawaida kwa Serikali ya Uingereza mwaka jana Waziri Mkuu David Cameron alitangaza Uingereza kuanza kutumia kanuni za uchumi za kiislamu.

Ripoti iliyotolewa na Gazeti hilo mwaka 2013 ilidai baada ya miaka 20 nchi ya Uingereza itakuja kuwa nchi ya Kiislamu kutokana na kuongezeka idadi kubwa ya watu wanaoingia Dini ya Kiislamu nchini humo.