Gazeti la kila wiki la Yushaloom linalochapishwa huko Israel limeandika kuwa, viongozi wa Kiyahudi wa Baraza la Mji wa Quds wako mbioni kuweka mkakati wa kuweka sheria ya kupunguza sauti za adhana katika miezi ya hivi karibuni kwa kisingizio kuwa wakazi wa eneo hilo wanakerwa na kukosa utulivu kutokana na sauti za adhana kuwa kubwa.
Baraza la Mji wa Quds limetangaza kuwa, msikiti ambao hautatekeleza amri hiyo ya kupunguza sauti ya adhana, utaorodheshwa kwenye orodha nyeusi.
Sheikh Azzam al- Khatib ambaye ni kiongozi katika msikiti wa Al Aqsa alisema hiyo ni jitihada za kutokomeza utambulisho wa Kiislam katika ardhi yao na kupindua utamaduni wa Kiislamu katika mji mtakatifu.
Utawala wa Israel mara kadhaa umekuwa ukipiga marufuku kuadhiniwa kwenye misikiti ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
![]() |
| Masjid Al-Aqsa |
