Wednesday, 5 March 2014

UJENZI WA JENGO LA WESTGATE WAANZA

Ujenzi wa jengo la maduka mengi la Westgate jijini Nairobi ulianza siku ya Jumatatu wiki hii, ikiwa ni miezi mitano baada ya wanamgambo wa Al-Shabaab kulishambulia jengo hilo na kuuwa watu 67 huku jengo lenyewe likiathirika vibaya.

Kamati ya Ujenzi wa Haraka wa Westgate liliwasilisha ripoti yake ya kurasa 74 kwa Waziri wa Biashara na Utalii, Phyllis Kandie, siku ya Jumatatu. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, David Muigua, alisema alitazamia jengo hilo kuanza tena uendeshaji muda si mrefu.

"Siwezi kusema tarehe hasa ya jengo hilo litakapofunguliwa. Ninaweza tu kusema kuwa ripoti itakuwa na ufafanuzi wa mambo hayo ya ratiba ya wakati," alisema.

Kazi za ujenzi huo mpya zitagawiwa kati ya ujenzi kamili wa maeneo yaliyoharibiwa na uimarishaji wa haraka zaidi wa maeneo ambayo yalikuwa salama kiujenzi.

"Sehemu ya juu ya kuegesha magari ya duka la Nakumatt, ambayo iliathirika vibaya, itajengwa kuanziwa awali kabisa ambapo maeneo mengine yatafanyiwa marekebisho kabla ya biashara kuruhusiwa kuanza tena," alisema Muigua.


Muonekano wa Wastgate kabla ya kuvamiwa