Wednesday, 5 March 2014

ARNOUD VAN DOORN AANZISHA CHAMA CHA SIASA CHA KIISLAMU NCHINI HOLAND

Mwanasiasa mashuhuri wa kiholandi aliyesilimu Arnoud Van Doorn ametangaza kuanzisha chama cha siasa cha kiislamu nchini Holand hivi karibuni.

Chama hicho kitakachojulikana kwa jina la 'Islamic Party for Unity' kinatarajiwa kushiriki katika uchaguzi wa kugombea viti vitatu vya halmashauri mnamo mwezi marchi 19.

"Katika mji wenye waislamu 100,000 hadi 150,000 hakuna zaidi ya mantiki kwamba wao pia wawe na uwakilishi wa kisiasa", alisema katika mahojiano na Algemeen Dagblad wa NL Times Jumapili .

Alisema msingi wa chama hicho ni kuwa na uwakilishi wa kisiasa kwa waislamu ambao ni wachache nchini Holand.
"Sehemu kubwa ya wafuasi wetu ni Waislamu, hivyo bila shaka sisi pia tutakuwa kwa ajili yao", aliongeza.

Doorn alisema kuwa chama chake hakipaswi kuchukuliwa ni chama cha kiislamu, lakini kitakuwa na itikadi za Kiislamu.

Alipoulizwa msimamo wa chama chake na masula ya ushoga alipinga suala hilo kwa kusema chama chake hakikubali ushoga kwani itikadi ya uislamu inapinga jambo hilo.

Arnoud Van Doorn mwanachama wa zamani wa chama cha right Freedom Party (PVV) alisilimu mwanzoni mwa mwaka jana baada ya kuufanyia utafiti wa kina wa Uislamu.

Kabla ya kusilimu Arnoud van doorn ndiye aliyekuwa kinara wa kumpinga na kumkashifu Mtume. Van Doorn amesaidia kutoa filamu ya kumkashifu Mtume ﷺ iliyoitwa 'Fitna'.

Baada ya kupingwa sana  kwa filamu hiyo na waislamu kulimfanya Van Doorn kuufanyia utafiti uislamu ambako kulimpelekea kusilimu kwake.

Van doorn baada ya kusilimu alienda kufanya ibada ya Umra na kuzuru kaburi la Mtume ﷺ, alifanya maombi maalumu ya msamaha kwa kumkashifu Mtume .

Japo aliambiwa haina haja kufanya toba kwa kuwa kusilimu kwake ni toba tosha kwa yale aliyoyatenda. Lakini Van Doorn alisema kufanya hivyo ni bora kwake kwani kutamsaidia utulivu ndani ya nafsi yake.

Mbali na ibada ya Umra pia amehudhuria hijja ya mwaka jana. Aidha kusilimu kwa Arnoud Van Doorn kumewafanya watu wengi kuvutika na uislamu na kupelekea kusilimu kwa makundi ya watu wa Ulaya. 

Kwa mwaka inakadiriwa kusilimu watu 15,000 nchini Holand tangu kusilimu kwake. Waislamu nchini Holand wanakadiriwa kufikia milioni moja.


Arnoud Van Doorn (kulia)