"Tumeng'amua kwamba ni vigumu kuulinda mpaka huu mrefu na wenye matatizo. Tutahakikisha hilo linafanyika na tutashungulikia tatizo la kimsingi la al-Shabaab nchini Somalia," alisema Godec kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.
Marekani pia itaisaidia Kenya katika kukabiliana na upandikizaji wa siasa kali nchini na kitisho kinachoonekana cha ugaidi wa ndani.
"Tuna wajibu wa kusimama pamoja na Wakenya na dhamira yetu ni kusaidia kulikabili suala hili," alisema.
Godec alisema Shirika la Ujasusi la Marekani linavisaidia vyombo vya usalama vya Kenya kuchunguza kesi za ugaidi, na kuitolea wito serikali ya Kenya kutumia njia ya mazungumzo na vijana ambao hawaridhiki na hali ilivyo ili kuumaliza upandikizaji wa siasa kali akirejelea mkasa kutekwa na hatimaye mauaji kwenye msikiti hivi karibuni mjini Mombasa.
"Umefika wakati wa kuwaleta wale wanaoshukiwa [kupandikizwa siasa kali] karibu zaidi na kuwapa elimu nzuri," alisema.
![]() |
| Robert Godec |
