Hayo yamesemwa na Sheikh Yusuf Kidago akiongea katika kipindi cha 'jukwaa kwa asiye na jukwaa' kinachorushwa na Redio Kheri.
Aidha, Sheikh Yusuf amesisitiza kwamba madrasa ndio mkombozi wa maadili na akili za watu kwani kwa kupitia madrasa watu watamuogopa mwenyezi Mungu na hawatafanya matendo machafu kama Ushoga na Usagaji.
Alisema kwa sasa dunia inakabiliana na changamoto kubwa ya uhimizwaji wa Ushoga hivyo dawa ya kudhibiti hali hizo ni kuimarisha madrasa na kila mzazi kumpeleka mtoto wake ili aweze kujengwa katika maadili mema na kujiepusha na maadili yasiyo mazuri.
"Madrasa inasimamia malezi bora, inasaidia kujenga khofu na kujenga jamii nzuri", alisema Sheikh Yusuf.
Aliongeza kusema kwa sasa jamii ina mmomonyoko wa maadili kwa vijana wengi kuiga watu wamagharibi kwa vijana wa kiume kuvaa hereni na mkufu, kusuka nywele, kuvaa suruali chini ya makalio na wanawake kuvaa mavazi ya kiume.
![]() |
| Sheikh Yusuf Kidago |
Kwa sasa Duniani imeingia katika shinikizo kutoka kwa nchi za Amerika na ulaya kutaka nchi zingine zitambue haki za mashoga.
Tayari nchi ya Uganda imeingia kwenye misukosuko baada ya kupitisha sheria kali dhidi ya Mashoga kwa yeyote atakayebainika kufungwa jela maisha.
