Monday, 10 March 2014

SAUDI ARABIA YATANGAZA KUWA IKHWANUL MUSLIMIN NI KUNDI LA KIGAIDI

Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umetangaza rasmi kuliweka kwenye orodha ya makundi ya kigaidi kundi la Ikhwanul Muslimin la Misri .  

Uamuzi huo ulitangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia Arabia kwamba ni marufuku kupewa msaada au kuungwa mkono au kufanya muamala wa aina yoyote na kundi hilo.

Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa hairuhusiwi ndani ya Saudi Arabia kufanywa mikutano ya kuliunga mkono au kulitangaza kundi hilo la Ikhwanul Muslimin.