Monday, 10 March 2014

NIGER YATAKIWA KUTHIBITISHA MTOTO WA GADDAF ANATENDEWA HAKI

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu katika eneo la mashariki ya kati na Afrika kaskazini wameitaka Niger kuelezea uamuzi wake wa kumshtaki mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muamer gaddafi Saad Gaddafi, ambapo Ofisi ya mwendesha mashtaka mjini Tripoli imesema kuwa anakabiliwa na tuhuma za kumsadia baba yake kusalia madarakani kinyume cha sheria.

Mkurugenzi wa shirika la la kutetea haki za binadamu la kimataifa la Human Right Watch  lenye makao yake makuu huko New York Marekani Sarah Leah Witson ameitaka Niger kuthibitisha kuwa Saadi Kadhafi hatafanyiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na haki itatendeka kwa mujibu wa sheria.

Aidha shirika hilo limeikumbusha serikali ya Libya kuhakikisha linafuatilia Saad Gadafi kupata haki zake ikiwemo kumlinda dhidi ya mateso na ukatili,kuruhusiwa kutembelewa na washauri wa kisheria,familia yake na wahudumu wa afya na kumfikisha mbele ya makahama mapema iwezekanavyo.

Hofu kuhusu usalama na hatma ya Saad Gaddafi mtoto wa aliyekuwa mtawala wa Libya, marehemu kanali Muamar Gaddafi imekuwa ni sintofahamu kufuatia tuhuma za mateso wanayofanyiwa wafuasi wa kiongozi huyo walioko kizuizini.

Hofu hii inakuja mara baada ya utawala wa Niger kutangaza kumkabidhi kwa mamlaka za Libya, mtoto wa marehemu kanali Gaddafi, Saadi Gaddafi aliyekuwa akiishi uhamishoni toka kuangushwa kwa utawala wa baba yake.

Kikosi cha wanajeshi ambako mtoto huyo anashikiliwa mjini Tripoli, kimechapisha picha kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook zikimuonesha mmoja wa askari hao akimnyoa nywele kwa nguvu Saad Gaddafi huku akiwa amepiga magoti.
Sarah Leah Witson