Tuesday, 4 March 2014

ROBOTI MAALUM LAZINDULIWA KWA AJILI YA KUFUNDISHIA WANAFUNZI NAMNA YA KUSALI

Roboti maalumu kwa ajili ya kufundishia wanafunzi namna ya kujua kufanya ibada ya swala limezinduliwa rasmi huko Tehran nchini Iran.

Roboti hiyo imezinduliwa na mwalimu Akbar Rezaie mwenye umri wa miaka 27 anayefundisha katika shule ya Alborz iliyopo Varamin karibu na Tehran. 

Roboti hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa vijana wadogo kujifunza namna ya kusali kwa njia iliyo rahisi zaidi. 

Roboti hiyo Akbar Rezaie ameitengeneza nyumbani kwake na kuifanyia marekebisho makubwa kiasi cha kuweza kusujudu na vitendo vingine vya swala.

Akbar Rezaie alipenda kutengeneza Roboti la namna hiyo ili kuwasaidia wanafunzi wake. Hivyo aliamua kwenda kujifunza namna ya utengenezaji Roboti kabla hajaliunda la kwake.

Roboti maalum ikiwafundisha wanafunzi matendo ya swala