Friday, 7 March 2014

NIGER YAMKABIDHI MTOTO WA GADDAF, SAAD KWA SERIKALI YA LIBYA

Serikali ya Niger imesema kuwa, imemkabidhi Saad Gaddafi kwa serikali ya Libya baada ya mazungumzo ya pande mbili. 

Saad Gadafi, mwana wa zamani wa kiongozi wa Libya aliyeuawa, Muammar Gaddafi aliikimbia Libya na kuelekea Niger baada ya kupamba moto mapigano yaliyomuondoa madarakani baba yake mwaka 2011. 

Serikali ya Libya imethibitisha kuwa Saad amewasili Tripoli na kwa sasa anashikiliwa kwenye gereza moja mjini hapo.

Huko nyuma Niger ilikuwa imekataa kumkabidhi Saad kwa serikali ya mpito ya Tripoli lakini baada ya mazungumzo mapana ya pande mbili, Niamey imekubali kumkabidhi mwana huyo wa kiume wa kanali Gadafi. 

Saad anakabiliwa na mashtaka ya kuwaua watu kwa kuwapiga risasi alipokuwa mkuu wa kikosi maalumu cha jeshi wakati wa utawala wa baba yake.