Friday, 7 March 2014

KANSELA WA CHAMA CHA CONSERVATIVE ALIYEKASHIFU BURQA ASIMAMISHWA UANACHAMA KWA MWAKA MMOJA, ATOLEWA KUGOMBEA KATIKA UCHAGUZI

Kansela wa Enfield katika jijini la London nchini Uingereza Chris Johannides amefungiwa kwa muda wa mwaka mmoja kujishghulisha na chama chake cha Conservative kufuatia kufanya dhihaka na kukashifu vazi la kiislamu la Burqa.

Chris Johannides ambaye ana asili ya kigiriki pia ameondolewa katika nafasi ya kugombea kupitia chama chake katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu. 

Maamuzi hayo yamekuja kufuatia kuweka picha katika akaunti yake ya facebook inayomuonesha mwanamke wa kiislamu akiwa na mtoto wake wa kike wamesimama karibu na mifuko myeusi ya kuhifadhia taka huku akimlinganisha binti wa kiislamu aliyevaa Burqa na mifuko hiyo myeusi ya Plastiki inayohifadhia taka. 

Msemaji wa Conservative, alisema chama kimemsimaisha Chris Johannides uanachama kwa muda wa miezi 12 na hakuna rufaa inayoruhusiwa chini ya sheria za chama. 

Chris Johannides ambaye mwaka 2006 alipochaguliwa kuwa Kansela aliweka rekodi ya kuwa Kansela mdogo kuchaguliwa nchini Uingereza. 

Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 26. Mwaka jana alitajwa kama mmoja wa watu wanaoupiga vita na kuuchukia sana Uislamu huko Uingereza.


Picha aliyoiweka na maelezo aliyoyasema
Chris Johannides