Kampuni ya Glocall Telecoms inapanga kutoa uunganishaji wa simu za mkononi na intaneti ya 4G LTE yenye kasi kubwa kwa wakazi wa mjini Mogadishu, afisi za serikali, shule na wafanyabiashara, kampuni shirika ya Tazca Connects ilitangaza siku ya Jumatano.
"Kupeleka 4G LTE na Tazca kConnects utazidisha kasi ya kuunganishwa kimataifa katika Somalia na kutoa fursa mpya za kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kijamii kwa kuongeza upatikanaji wa habari na huduma zenye kiwango", afisa mtendaji mkuu wa Glocall Telecoms Mubin Bhamjee alisema katika taarifa.
Tazca Connects itatumia jukwaa la software kutoka kampuni ya Lemko Corporation ambalo litaleta uunganishwaji kwa biashara na jamii za Mogadishu.
"Ushirikiano wetu nchini Somalia unaonyesha kuwa programu yenye nguvu, pamoja na dira yenye nguvu, vinaweza kuwaunganisha watu mahali popote duniani kwa gharama nafuu, huduma za LTE za daraja la juu," alisema Michael Sisto, makamo raisi wa mauzo wa Tazca.
"Tumefurahishwa kwa kuonesha kwamba, pamoja na Tazca, faida ya kiuchumi na kijamii ya kupanua upatikanaji wa mtandao vinaweza kuwa ukweli wenye nafuu katika jamii yoyote."
Tangazo hilo linakuja kufuatia marufuku ya Al-Shabab juu ya intaneti kwa njia ya simu za mkononi huko kusini na kati ya Somalia, ikiwemo Mogadishu.
Kampuni za Glocall Telecoms na Tazca Connects zote ni watoaji wa huduma za mawasiliano ya simu zenye makao Marekani zinazolenga barani Afrika na maeneo mengine yenye huduma duni.
.jpg)