Monday, 17 March 2014

MISAADA YA IRAN KWA WAISLAMU WA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI YAFIKA CHAD

Shehena ya kwanza ya misaada ya kibinadamu kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati imewasili kwenye kambi ya wakimbizi wa nchi hiyo iliyoko nchini Chad. 

Shehena hiyo iliyotumwa na Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran inajumuisha mahema, mablanketi, madawa na vyakula imetumwa kwa wakimbizi wa Kiislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaopewa hifadhi nchini Chad. 

Taarifa zinasema kuwa, msaada huo wa kibinadamu kwa Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati umepelekwa na ndege maalumu nchini Chad.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada ya kibinadamu yameingiwa na wasiwasi wa kujitokeza balaa la njaa na mauaji ya kimbari yanayofanywa na wanamgambo wa Kikristo wa Anti Balaka dhidi ya Waislamu nchini humo.