Monday, 17 March 2014

MAKAO MAKUU YA JESHI LA SERBIA LAWAJENGEA JENGO LA IBADA ASKARI WAKE WAISLAMU

Jeshi la nchi ya Serbia limefungua jengo maalum la kusalia kwa ajili ya Askari wake waislamu walioko makao makuu ya jeshi hilo huko Belgrade.

Mkuu wa wafanyakazi Ljubisa Muhamed Jusufspahić ambaye  alishiriki katika sherehe za ufunguzi wa jengo hilo siku ya alhamisi alisema wamefurahishwa na hatua hiyo na ni ishara inayoonesha njia ya kuthamini watu wa dini.

Hii ni hatua ya pili ambapo jengo  lingine kwa ajili kufanyia ibada kwa Askari wa Serbia lilifunguliwa katika mji wa Novi Pazar.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2011 uislamu ni dini ya tatu baada ya watu wa madhehebu ya Orthodox na wakristo.

Waislamu ni asilimia 3.1 (220,828) kati ya watu milioni 7.1 wa nchi ya Serbia.