Saudi Arabia imetoa orodha ya majina takriban 50 ambayo imeagiza wasipewe watoto wanaozaliwa nchini humo.
Wizara ya masuala ya ndani nchini humo ilisema marufuku hiyo ilitokana na hali kwamba majina hayo baadhi yanaenda kinyume na utamaduni na dini ya taifa hilo, ni ya kigeni, au ‘hayafai’.
Orodha kamili ya majina hayo yaliyokatazwa nchini Saudi Arabia ni:-
Malaak (angel/malaika), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Benjamin),Naris,Yara,Sitav,
Loland,Tilaj,Barrah,Abdul Nabi, Abdul Rasool, na Sumuw (highness/Muadhama).
Mengine ni Malika (queen/malkia), Al mamlaka (kingdom/ufalme), Tabarak (blessed/mbarikiwa), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god/mungu wa kihindi), Maline, Elaine, Inar, Maliktina, Maya, Linda, Randa, na Basmala (utterance of the name of God/tamko la jina la Mungu).
Mengine ni Jibreel (angel Gabriel), Abdul Mu'een, Abrar, Iman, Bayan, Baseel, Wireelam, Nabi (prophet), Nabiyya (female prophet/nabii wa kike), Amir (Kiongozi)
Taline, Aram, Nareej, Rital, Alice,Lareen, Kibrial, na Lauren.