Wakati mkutano wa baraza la haki la Umoja wa mataifa ukiendelea mjini GenevaUswisi, Tanzania imesema ufutwaji wa hukumu ya kunyonga nchini humo kunategemea maoni ya wananchi na kwamba mchakato huo unaendelea licha ya shinikizo kutoka jumuiya ya kimataifa.
Akizungumzia ripoti ya hali ya haki za binadamu iliyowasilishwa katika mkutano huo, mwakilishi wa kudumu waTanzaniakatika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Balozi Modest Mero amesema nchi yake imekuwa ikizingatia demokrasia kwa kuwashirikisha wananchi kwa kila hatua ikiwamo masuala nyeti kamahilo.
Amesema wananchi wamekuwa bado wanasita kuondolewa kwa hukumu hiyo kwa hofu ya ukatili juu wahalifu kuongezeka zaidi.
Aliongeza kusema kuwa jibu lao kwa umoja wa Mataifa ni mpaka wananchi waridhie wenyewe kuondolewa kwa adhabu hiyo.
Hata hivyo Balozi Mero amesema wizara ya Katiba na Sheria ndiyo inaratibu mchakato huo.
