Monday, 3 March 2014

KWA MARA YA KWANZA MSIKITI WA MAKKAH WATOA KHUTBA YA IJUMAA KWA LUGHA ZA KIINGEREZA NA KIURDU

Kwa mara ya kwanza Msikiti Mtakatifu wa Makkah 'Masjid Haram' Ijumaa iliyopita imetoa khutba ya ijumaa kwa Lugha za Kiingereza na kiurdu.

Khutba yenyewe ilikuwa ya kiarabu kama kawaida ila waumini walipewa 'earphones' zilizokuwa zikitafsiri kwa lugha hizo mbili kwa wale wenye kuelewa lugha hizo. 

Utaratibu huu ni katika kuwasaidia wale wote wasio kuwa na uelewa wa lugha ya kiarabu ili nao waweze kufahamu nini kimezungumzwa katika khutba za Ijumaa.

Mpango huo mpya kwa sasa ni wa majaribio katika msikiti huo ambapo mpango wa baadae ni kupeleka huduma kama hiyo katika Msikiti wa Mtume Muhammad  Masjid Nabawi,Madina.


Masjid Haram