Sunday, 2 March 2014

AL-SHABAB WAONYA WAKAZI WA MOGADISHU DHIDI YA MASHAMBULIZI ZAIDI

Wakaazi wa Mogadishu wanapaswa kukaa kando na majengo ya serikali kwani kundi la Al-Shabaab linapanga kufanya mashambulizi zaidi, alisema kamanda wa kundi hilomkoani Benadir, Ali Mohamed Hussein.

"Wakaazi wote wa Mogadishu lazima wakumbuke kukaa mbali na majengo ya serikali, ili wasidhurike wakati wa mashambulizi dhidi ya adui wetu," alisema Hussein kwa mujibu wa Horseed Media.

Onyo hilo linafuatia bomu lililotegwa kwenye gari kulipuka siku ya Alhamisi katika mgahawa mmoja karibu na makao makuu ya Shirika la Ujasusi la Somalia mjini Mogadishu na kuua watu 12.


Al-Shabab