Masjid Aljumuiyyatil Islamiyya maarufu kama Msikiti wa Kisumu uliopo Magomeni Mikumi, jijini Dar Es Salaam jumamosi walifanya Kilele cha sherehe za mazazi ya Mtume Muhammad ﷺ msikitini hapo.
Sherehe hizo zilianza siku ya Alhamis kwa Maonesho ya wanafunzi pamoja na Maulid ya kinamama. Ijumaa ilikuwa ni samai.
Katika kilele cha sherehe hizo Masheikh mbalimbali walihudhuria wakiongozwa na Kadhi Mkuu wa Tanzania Sheikh Abdallah Mnyasi.