Sunday, 9 March 2014

KENYA YAZINDUA MTAALA MAALUMU WA UFUNDISHAJI MADRASA, NIA NI KUONDOA MISIMAMO MIKALI

Mtaala mpya unafanyiwa majaribio katika shule 50 za kidini nchini Kenya ukiwa na lengo la kuboresha masomo ya Kiislamu na kuhakikisha mafundisho ya misimamo mkali hayapandikizwi katika madrasa.

Utayarishaji wa mtaala huo mpya ulikuwa ni juhudi za pamoja zilizoongozwa na Al-Muntada al-Islami Trust, shirika la misaada la kimataifa lenye makao yake nchini Uingereza, kwa kushirikiana na Baraza la Wasomi wa Kiislamu nchini Kenya, Baraza Kuu la Waislamu Kenya na wawakilishi kutoka Taasisi ya Uendelezaji Mitaala ya Kenya (KICD).

Alisema Sheikh Abdilatif Abdulkarim, mjumbe wa bodi wa al-Mutanda al-Islami Trust mjini Nairobi kwamba kushindwa kuwa na mtaala mmoja wa masomo ya Kiislamu umeacha mapengo ambayo wakuu wa dini wenye jazba wamekua wakiitumia kuwafanya vijana wawe na misimamo mikali.

"Nadhani hii ni njia mojawapo ya kukabiliana na misimamo mikali," alisema. "Kwa mtaala huu, tutakuwa na uwezo wa kufanya walimu wa madrasa kutoa vitu ambavyo ni muhimu kwa watoto, na itakuwa rahisi kuwawajibisha wale ambao wanapinga kanuni kupitia tathmini."

Mtaala huu, ambao ulichukua miaka mitatu kuutengeneza, pia utajumuisha masomo ya maadili ya kuvumiliana na umuhimu wa utaifa, alisema.

"Mbali na kufuata Uislamu, tunahitaji watoto hawa wawe wazalendo kwa taifa lao na upendo kwa raia wengine bila kujali imani zao wakati watakapokua wakubwa," alisema. 

"Ni kwa njia ya elimu tu tunaweza kupata stadi hizo, ndio sababu tumeingiza [masomo hayo] katika mtaala. Hiyo kitafanya kuwa vigumu kwa wao [watoto] kuangukia kwenye mikono ya wahalifu kama vile magaidi", aliongeza.

Mpango wa majaribio ya siku 90 ulianzishwa tarehe 6 Februari katika Shule za Mombasa, Nairobi na Garissa ambazo zinashiriki kwa hiari, alisema Abdul Karim, akiongeza kuwa wana matumaini ya kutumia mtaala huo kote nchini ifikapo mwezi Januari 2015.

Mwanasheria Ibrahim Lethome, ambaye alisaidia kuandika mtaala mpya na kwa sasa anafanya kazi ya kuutekeleza, alisema kulikuwa na haja ya haraka ya kuunganisha na kuwianisha masomo ya Kiislamu katika shule binafsi za kidini kwa vile Wizara ya Elimu ya Kenya inazitambuwa rasmi.

"Tumekuwa na ombwe katika eneo hili, na kwa hiyo mtaala huu ni hatua kuelekea kujaza ombwe hilo na kuona taasisi hizi zinakubiliana na mahitaji yetu ya kufundishia," alisema Lethome, mtaalam wa sheria ya Kiislamu na mwanachama wa Kamati ya Msikiti Jamia wenye makao yake Nairobi.

"Tunachofanya sasa ni kupima programu hii katika mradi wa majaribio," alisema. "Katika roho ya ushiriki wa wananchi, katika kipindi hiki, tutaweza kupata maoni ya wazazi na wadau wengine juu ya vipi mtaala unapaswa uwe."

Kabla ya mtaala huu kupitishwa kwa ajili ya kutumika nchi nzima, programu ya majaribio itafanyiwa tathmini na uwezekano wa kurekebshwa, alisema Abdi Kheir, ofisa programu katika KICD, chombo cha serikali chenye dhamana ya kutathmini na kuidhinisha mitaala ya shule za Kenya katika kiwango cha chini ya chuo kikuu.

"Kwa jumla, hii ni hatua kubwa katika mwelekeo sahihi na hatimaye itabadilisha jinsi masomo ya Kiislamu yanavyofundishwa nchini," alisema.

Kuwa na mtaala unaojulikana na kupitishwa itasaidia kuondoa tuhuma zisizofaa kutoka kwa wananchi wenye mashaka na yale yanayoendelea katika shule zisizo rasmi, alisema. "Hii itasaidia kukuza maelewano na kukubaliana."

Alisema Wakati wa majaribio ya tathmini, KICD itaendelea kutoa msaada wa kiufundi. Mara baada ya mtaala wa mwisho ni kupitishwa, madrasa zinatakiwa kuupitisha kama sharti kabla ya kupokea leseni ya kuendesha shughuli zao.

Kwa upande wake, Sheikh Abu Hamzah, imam wa Msikiti Huda huko Mombasa, aliusifia mtaala huo kwa kusema kuwa utaleta usawa katika utoaji wa vitu vinavyohitajika na kuisaidia jamii kuendeleza mifumo ya pamoja ya kidini kwakutatua mizozo yao.

Mtaala huo mpya pia unatoa miongozo kwa ajili waelimishaji juu ya mbinu za kufundishia, alisema Hamzah, ambaye shule yake inashiriki katika majaribio.

"Mtaala unayo mazoezi ya ufundishaji kwa sisi waelimishaji, kuanzia jinsi ya kupanga [masomo], na kupanga ratiba za kila siku za kufundisha na maudhui ya mtaala kwa kila kikundi cha umri, ikiwa na maana kuwa tutakuwa na utaratibu katika mitazamo yetu, na hivyo kuepuka kupoteza muda," alisema.