Saturday, 8 March 2014

UTURUKI YAJENGA MSIKITI MKUBWA ZAIDI ASIA YA KATI KATIKA NCHI YA KYRGYZSTAN

Wizara ya mambo ya dini ya Uturuki inafanya kazi ya kukamilisha ujenzi wa msikiti utakao kuwa mkubwa zaidi kuliko yote katika eneo la Asia ya kati katika mji mkuu wa nchi ya Kyrgyzstan, Bishkek.

Ujenzi wa msikiti huo ulianza machi 2012 umejengwa juu ya ardhi ya ekari 5 na ukubwa wake ni mita za mraba 1,300. Msikiti huo utakuwa na minara minne, miwili tayari imeshakamilika. 

Pia kunajengwa eneo la kuchukulia udhu lililokubwa zaidi,
sehemu ya kuegeshea magari mia nane kwa wakati mmoja pamoja na ofisi ya Mufti. Ujenzi unatarajiwa kukamilika mwaka 2015.


Ujenzi ukiendelea