Chama hicho kinachotarajiwa kuzinduliwa kinaitwa Australian Liberty Alliance. Katika uzinduzi huo Geert Wilders anatarajiwa kuzungumzia 'Uislamu na Migogoro' ambapo mada hiyo itaonesha hatari na wasiwasi wa maandamano ya waislamu katika nchi za magharibi.
Geert Wilders ndiye aliyeandaa na kutengeneza filamu ya 'Fitna' iliyokuwa ikimkashifu Mtume Muhammad ﷺ akishirikiana na aliyekuwa rafiki yake kipenzi Arnoud Van Doorn ambaye kwa sasa amesilimu na ameanzisha chama cha kiislamu nchini Holand.
Disemba mwaka jana Geert Wilders alifungiwa akaunti yake na google, baada ya kutolewa malalamiko dhidi yake kwa kutumia akaunti hiyo kueneza chuki ya kupambana dhidi ya Uislamu.
Malalamiko hayo yaliwasilishwa na Mohammed Rabbae kwa niaba ya Baraza la taifa la Morocco kwa kutumia vibaya huduma za Google. Malalamiko ya Rabbae yalitokana na malalamiko ya watu wengi dhidi ya Wilders kufuatia kutoa stika iliyosomeka kwamba, 'Uislamu ni uongo, Muhammad ana kosa la jinai, Qurani ni Sumu'.
Wilder ndiye mtu anayetajwa kwa sasa kuongoza kuwa na chuki zaidi dhidi ya Mtume Muhammad ﷺ na dini ya Uislamu.
![]() |
| Geert Wilders |
