Friday, 14 March 2014

AL SHABAB WATEKA KITUO CHA UMEME HUKO EL BUR, WAKATA UMEME NA MAJI

Al-Shabaab wameteka kituo cha umeme ambacho kinasamabaza umeme katika wilaya ya El Bur mkoani Galgadud, na kingine ambacho kilikuwa kinasukuma usambazaji wa maji kwa wakazi wa ndani, Naibu mwenyekiti wa kamati ya Utendaji ya Ahla Sunna Wal Jamaa Sheikh Ahmed Abdullahi alisema.

Wanamgambo hao waliripotiwa kuharibu majenereta yote na vifaa vingine muhimu katika uvamizi wao siku ya Jumapili.

"Wilaya ya El Bur mkoani Galgadud iko katika hali ngumu," alisema. "Wakati adui al-Qaida na al-Shabaab ambao wana makaazi hapo waliposikia kuhusu mashambulio ya [kijeshi] yanayowasogelea, waliamua kusababisha hali ngumu kwa watu."

"Ugumu wa hivi karibuni kwa sasa uko katika pande tatu," alisema. "Upande wa kwanza ni kwamba wamekata umeme jijini. Upande wa pili walichukua jenereta ambayo ilikuwa inasambaza maji katika mji huo, na upande wa tatu wanawalazimisha watu kukikimbia jiji hilo kwenda mashambani wakati huu wa msimu wa joto."

Abdullahi alisema mpango huo wa kukomboa raia kwa msaada wa vikosi vya Ethiopia vinavyofanya kazi chini ya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) ulifungwa.

Viongozi wa Al-Shabab