Thursday, 6 March 2014

AL-SHABAB YAWAUA WASOMALI WATATU KWA TUHUMA ZA UJASUSI

Al-Shabaab imewaua watu watatu huko Barawe Jumanne wakiwatuhumu wawili kati yao kufanya ujasusi kwa ajili ya serikali ya Somalia na utawala wa Puntland na mwingine kwa ujasusi kwa ajili ya Ufaransa na Marekani.
Mohammed Abdulle Gelle, mwenye umri wa miaka 29, alituhumiwa kusaidia shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani huko Jilib mwezi Oktoba 2013 ambalo ilisababisha makamanda waandamizi wawili wa al-Shabaab kuuawa.
Al-Shabaab ilitangaza katika ukurasa wa Facebook wa Redio Andalus. Gelle pia alituhumiwa kufanya kazi kwa ajili ya jeshi la Ufaransa ambalo lilitekeleza uvamizi dhidi ya Al-Shabaab huko Bulomarer mwezi Januari 2013.
Ahmed Abdullahi Farole, mwenye umri wa miaka 47, alituhumiwa kwa kupeleleza utawala wa Puntland, na Abdirahman Abdulatif alituhumiwa kupelelezea shirika la upelelezi la taifa la Somalia.
Farole ni mpwa wa aliyekuwa Rais wa Puntland Abdirahman Mohamed Farole, Redio ya RBC ya Somailia iliripoti.
Watuhumiwa hao watatu waliuawa kwa kupigwa risasi na kikosi cha kuua waliotuhumiwa kifo baada ya jaji wa al-Shabaab kutamka kuwa wana hatia.