Friday, 14 March 2014

BENDI YA MUZIKI KOREA KUSINI YATAKIWA KUTOA AYA ZA QURANI ZILIZOTUMIKA KATIKA WIMBO WAO MPYA

Bendi ya wanamuziki wa kike wa korea kusini ya 2NE1 imewakasirisha waislamu wa nchini humo baada ya kugundulika imetumia aya za Qurani Tukufu katika moja ya mashairi ya wimbo katika albamu yao mpya iliyotolewa hivi karibuni.

Shirikisho la waislamu nchini korea kusini limeitaka bendi hiyo kuomba msamaha kwa matumizi mabaya ya Aya za Qurani na kurekebisha wimbo huo kwa kutoa Aya hizo katika wimbo huo.


Aya zilizotumika katika wimbo huo ni za 32 mpaka 34 za sura ya 78 suratil Nnaba. Aya walizotumia ni;
  حَدَائِقَ وَأَعْنَابًا ﴿٣٢ وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا﴿٣٣ وَكَأْسًا دِهَاقًا ﴿٣٤

YG Entertainment kampuni ambayo imetengeza albamu ya bendi hiyo imesema ipo tayari kufuta sehemu hiyo ya wimbo
ulioingizwa aya za Qurani

Wanamuziki wa Bendi hiyo