Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé amesema Uganda ilikuwa nchi ya kwanza ya kiafrika kuvunja mipaka na kujumuisha makundi ya pembezoni katika kukabiliana na ukimwi lakini sheria hiyo sasa itatumbukiza kapuni mafanikio yote yaliyopatikana.
Ameitaka serikali ya Uganda kutupilia mbali muswada huo akieleza kuwa utakuwa na madhara kwenye afya ya kijamii kwani utafiti umeonyesha kuwa mashoga wanapobaguliwa, wanakuwa na hofu kusaka huduma za kinga au tiba dhidi ya Ukimwi.
Tafiti zinaonyesha uwezekano wa mashoga kupata ukimwi kuwa ni mara 13 zaidi kuliko jamii nyingine na hivyo UNAIDS inataka huduma zitolewe bila ubaguzi wowote.
Ahbaabur Rasuul: Tumeiweka habari hii ili uone wanaadamu wasiokuwa na muongozo wa dini akili zao zinavyofanya kazi. Kinachotetewa ni kile kilichofanya Mwenyezi Mungu aangamize kaumu ya nabii Luti. Na kwamba kuzuia ushoga kutaongeza maambukizi ya Ukimwi! Inna lillah wainna ilahi raajiun
![]() |
| Michel Sidibe |
