Akihutubia wanahabari, kasisi wa kanisa hilo, Bw Allen Parker, alisema walifikia uamuzi huo wa kuomba uchi baada ya kubainisha kuwa mavazi yana 'udanganyifu fulani’ na akaongezea kwamba hatua hiyo 'itawafanya waumini wote kuwa sawa bila kuwepo kwa utofauti wa kimapato’.
Kasisi huyo alisema hatua hiyo ina ithibati ndani ya Biblia huku akidai kuwa miujiza mingi katika Biblia ilitendeka wakati ambapo wahusika walikuwa uchi.
Kwa mfano, alisema Yesu Kristo alikuwa uchi aliposulubishwa msalabani na wakati alifufuka kutoka kaburini. Japo matakwa ya kuwa uchi ndani ya kanisa si lazima, wengi wa waumini wanaonekana kuitikia wito huo.
Baadhi ya waumini ambao hawapendi kusalia uchi wa mnyama kanisani wanavalia nguo za ndani.
Ambao wamekumbatia wito huo wanasema wamezoea kuwa uchi kanisani japo walikuwa wakiona haya siku za mwanzoni.
Pasta wa kanisa hilo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha runinga nchini humo, alisema anafuata nyayo za Yesu. “Wakati ambapo Yesu alipitia hatua muhimu maishani alikuwa uchi,” alidai Bw Parker.
“Alipozaliwa alikuwa uchi, aliposulubishwa alikuwa uchi na wakati ambapo alifufuka aliacha mavazi yake ndani ya kaburi. Ikiwa Mungu alituumba hivyo, Je, kuna hatia gani kuwa uchi kanisani?” aliuliza.
Mamia ya waumini wamekuwa wakivumilia msimu wa baridi kali kila siku ya Jumapili kusikiliza Injili huku wakiwa uchi wa mnyama.
Wakati huo huo, maelfu ya watu wamekuwa wakifurika kwenye kanisa hilo kupiga picha. Zaidi ya watu 10,000 huzuru kanisa hilo kila mwaka.
“Waumini wanapata fursa ya kusikiliza na kujadili Neno la Mungu,” alisema msimamizi wa kanisa hilo huku akiongezea kuwa kuna baadhi ya watu ambao wana mali nyingi huku wengine hawana kitu chochote.
Alieleza kuwa wanapoomba wakiwa uchi tajiri na maskini huwa sawa mbele ya Mungu.
![]() |
| Wakifatilia mahubiri |
![]() |
| Kanisa lenyewe |
![]() |
| wakiwa katika ibada |
![]() |
| waumini wakifungishwa ndoa |
![]() |
| kiongozi wa ibada |
![]() |
| wengine huacha wazi baadhi ya sehemu za mwili wao |
![]() |
| si lazima kuvua wengine huvaa nguo zao kama kawaida |






